Machapisho

VYETI KIDATO CHA NNE VYA WANAFUNZI 100 VYAYEYUKA

Picha
ZAIDI ya wanafunzi 100 waliohitimu kozi ya afya katika Chuo cha Sayansi ya Afya St. Aggrey jijini Mbeya, mwaka 2017, wamekilalamikia chuo hicho kwa kushindwa kuwarejeshea vyeti halisi vya kidato cha nne. Vyeti hivyo ni vile walivyotakiwa kukusanywa, kwa madai ya kwenda kuhakikiwa Wizara ya Afya. Hayo yamesemwa na Rais mstaafu wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Noeli Mng’ong’o. Alisema hayo alipokuwa akizungumzia adha wanazokumbana nazo, ikiwamo kukosa fursa za ajira serikalini na katika taasisi binafsi kutokana na ukosefu wa vyeti halisi vya kidato cha nne. Alisema mwaka 2015 wanafunzi 112 walijiunga na chuo hicho kwa kozi ya afya ngazi ya jamii kwa kipindi cha mwaka mmoja. Alisema uongozi wa chuo uliwataka wawasilishe vyeti halisi vya kidato cha nne ili vipelekwe Wizara ya Afya kwa ajili ya uhakiki, kama ni kweli walihitimu au la. Alisema tangu wakabidhi vyeti hivyo Novemba 2015, wamekuwa wakividai kwa uongozi wa chuo, lakini hadi sasa wamekuwa wakizun...

ALIYEBAKWA AKIWA NA MIAKA 70 ATAKA HAKI KUTENDEKA

Picha
MWANAMKE mmoja mkazi wa Mlodaa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Monica Tupa (70) amesema amekuwa akizungushwa tangu alipofanyiwa kitendo cha ubakaji Agosti mwaka huu na kuomba kusaidiwa ili haki iweze kutendeka. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto, alisema Agosti 14, 2017 alibakwa majira ya usiku akiwa nyumbani wake. “Ilipofika asubuhi nikaongozana na mjukuu wangu hadi kwa mkuu wa kitongoji kutoa taarifa, akaniambia nina hela gani ya kuendesha kesi, ikabidi tuondoke kwenda ofisi ya mtendaji tukakuta ofisi imefungwa,” alisema. Alisema mtendaji hakuwepo kijijini lakini aliporudi alimpa barua ya kwenda polisi kutoa taarifa wakati huo muda ulishakuwa umeshaenda sana. Alisema baadaye mtuhumiwa alikamatwa na kupelekwa polisi. “Nilipelekwa hospitali ya misheni ya Mvumi na waliponipima walinikuta na dalili zote kuwa nimebakwa,” alisema. Alisema kama serikali inataka kupunguza vitendo hivi ni muhim...

NJOMBE KUONGOZA KWA IDADI YA WATU WANAOISHI NA UKIMWI

Picha
Mkoa wa Njombe umetajwa kuongoza kuwa na asilimia 11.4 ya watu wanaishi na virusi vya Ukimwi huku Zanzibar wanaoishi na virusi hivyo ni chini ya asilimia 1. Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk Albina Chuwa ametoa takwimu hizo leo Desemba 1 katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambayo Kitaifa imefanyika viwanja vya Mnazi Mmoja. Dk Chuwa amesema mkoa wa Lindi umekuwa wa mwisho kwa watu wenye virusi  vya ukimwi na  idadi ya asilimia  0.1 huku maambukizo kwa Jiji la Dar es Salaam yamepungua hadi kufikia asilimia 4.7 ikiwa na maana watu 133,971 wanaishi na ugonjwa huo. Mkurugenzi huyo amesema kwa ujumla watu 1.4 milioni nchini Tanzania wanaishi na virusi vya Ukimwi na takwimu hizo ndiyo rasmi hivyo asitokee mtu au kikundi cha watu kupotosha. "Nasema kwa sababu kuna watu wanakurupuka na kuja na takwimu zao. Naomba watambue takwimu ni fani kama fani nyingine na zina miiko yake," amesema Dk Chuwa Hata hivyo, Dk Chuwa ame...

DUNIA YAADHIMISHA SIKU YA KUPAMBANA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI

Picha
Dunia inaadhimisha leo Ijumaa Desemba 1, siku ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi. Ugonjwa wa Sida umeendelea kuwaacha watoto wengi mayatima huku wengi wao wakiambukizwa ugonjwa huo na wazazi wao. Afrika Kusini ina idadi kubwa ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi duniani Watu milioni 17.1 wameambukizwa virusi vya Ukimwi nchini humo, kulingana na ripoti ya mwaka 2016. Baada ya miaka ya kadhaa, Pretoria imepata mafanikio makubwa katika kuzuia makali ya ugonjwa huo, vipimo na matibabu ya wagonjwa wa Ukimwi. Afrika Kusini ipo katika njia nzuri ya kufikia malengo yaliyowekwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalopiga vita Ukimwi (UNAIDS), ambalo linataka kuwa hadi mwaka 2020, 90% ya watu wanaoishi na VVU kujua hali yao, huku 90% ya watu walioathirika na VVU na waliopimwa, kupata matibabu na kwamba 90% ya wagonjwa wanaopata matibabu wawe wakipewa huduma ya kutosha. Mamlaka ya Afrika Kusini inakadiria kuwa 86% ya watu walio na VVU nchini humo wanajua hal...

RAIA WA NIGERIA WAUZWA KAMA MBUZI LIBYA

Picha
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema raia wote wa Nigeria ambao wamekwama Libya watarejeshwa nyumbani na kusaidiwa kurejelea maisha ya kawaida. Akizungumzia video za karibuni ambazo zimekuwa zikiwaonesha Waafrika wakiuzwa kwenye mnada wa watumwa nchini Libya, Rais Buhari amesema inasikitisha sana kwamba "baadhi ya raia wa Nigeria wanauzwa kama mbuzi - dola kadha Libya". Ameonekana pia kushangaa iwapo raia wa Libya walijifunza lolote la maana tangu kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011. ''Walichojifunza pekee ni kuwapiga watu risasi na kuua. Hawakujifunza kuwa mafundi wa umeme, mafundi wa mabomba au ufundi wowote ule," amesema. Kwenye video iliyotolewa na CNN mapema mwezi huu, vijana kutoka mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara walionekana wakiuzwa kama wafanyakazi wa mashambani kwa wanunuzi. Walikuwa wanauzwa $400 (£300) katika eneo ambalo halikufichuliwa Libya. ...

VIKAO VYA KUPANGA MADAKTARI YAANZA DAR

Picha
VIKAO kazi vya kujadili ili kuwapanga upya madaktari kwa uwiano, utakaoleta tija kwa nchi nzima na kuwahamishia madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwenda katika Kampasi ya hospitali hiyo ya Mloganzila, vimeanza kufanyika jijini Dar es Salaam. Uchunguzi wa gazeti hili uliofanywa, umebaini kuwa vikao hivyo vimeanza kufanywa na watendaji wa juu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kama utekelezaji wa haraka wa ushauri uliotolewa hivi karibuni na Rais John Magufuli. Rais Magufuli alitoa ushauri huo wakati akizindua Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Kampasi ya Mloganzila iliyopo wilayani Kisarawe, mkoani Pwani wiki iliyopita. Katika ushauri wake, Rais Magufuli alielezea nia yake ya kuona Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inalifanyia kazi suala hilo la kuwapanga vizuri zaidi madaktari katika mikoa yote nchini ili wananchi wapa...

FAIDA ZA KUFUATA RATIBA YA CHAKULA KWA AFYA BORA

Picha
FAIDA ZA KUFUATA RATIBA YA CHAKULA KWA AFYA BORA. Ili kuwa na afya njema ni muhimu kula vizuri . kula vizuri si rahisi ingawa wengi wetu tunadhani kula vizuri ni kula chips, kuku, au mayai na vingine haya ni mazoea mabovu. kula vizuri si lazima kula vyakula unavyovipenda bali ni kula vyakula vyenye afya na kujenga mwili wako. njia moja mbadala ya kuhakikisha unakula vizuri na kwa afya ni kuwa na ratiba ya wiki ya chakula. FAIDA ZA KUFUATA RATIBA YA CHAKULA. Kufahamu kirahisi ni vyakula vipi vyenye afya na mahitaji yako mfano mzuri ni kuwa na uwezo wa kula matunda na vyakula vya protini kwa wingi. Ni rahisi kujua virubisho muhimu unavyokula kwa kipindi cha wiki nzima hivyo ni rahisi kukusaidia kutathmini afya yako kwa uraisi. Kuwa na chaguo zaidi ya moja ya vyakula hivyo na kuzuia kula chakula cha aina moja kinachopendelewa na kusababisha kukosa virutubisho muhimu kwenye vyakula vingine. Kudumisha furaha nyumbani kwa sababu kila mmoja ataona umuhimu wake katika mawa...