Machapisho maarufu kutoka blogu hii
FAIDA ZA KUFUATA RATIBA YA CHAKULA KWA AFYA BORA
FAIDA ZA KUFUATA RATIBA YA CHAKULA KWA AFYA BORA. Ili kuwa na afya njema ni muhimu kula vizuri . kula vizuri si rahisi ingawa wengi wetu tunadhani kula vizuri ni kula chips, kuku, au mayai na vingine haya ni mazoea mabovu. kula vizuri si lazima kula vyakula unavyovipenda bali ni kula vyakula vyenye afya na kujenga mwili wako. njia moja mbadala ya kuhakikisha unakula vizuri na kwa afya ni kuwa na ratiba ya wiki ya chakula. FAIDA ZA KUFUATA RATIBA YA CHAKULA. Kufahamu kirahisi ni vyakula vipi vyenye afya na mahitaji yako mfano mzuri ni kuwa na uwezo wa kula matunda na vyakula vya protini kwa wingi. Ni rahisi kujua virubisho muhimu unavyokula kwa kipindi cha wiki nzima hivyo ni rahisi kukusaidia kutathmini afya yako kwa uraisi. Kuwa na chaguo zaidi ya moja ya vyakula hivyo na kuzuia kula chakula cha aina moja kinachopendelewa na kusababisha kukosa virutubisho muhimu kwenye vyakula vingine. Kudumisha furaha nyumbani kwa sababu kila mmoja ataona umuhimu wake katika mawa...
BIBI WA MIAKA 73 AOMBA TALAKA
MWANAMKE ambaye yupo kwenye ndoa kwa miaka 55, amefungua kesi mahakamani kuomba mumewe ampe talaka kwa madai kuwa hamjali, na anamthamini zaidi mke mdogo. Mwalimu huyo mstaafu, Marcella Mukami Kinyugo (73), anaiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kangema, isitishe ndoa yake na Peter Kinyugo (76) iliyofungwa Septemba 16, 1962 katika Kanisa Katoliki Kiriaini. Bibi huyo mkazi wa mjini Kiria-ini, Mathioya, kwenye kaunti ya Murang’a, pia aliomba apewe nusu ya mali za familia yao na pia mumewe alazimishwe kulipa gharama za kesi. Katika kesi hiyo bibi huyo aliwakilishwa na Margret Nyangati kutoka kampuni ya mawakili ya Muchoki Kang’ata. Aliieleza Mahakama kuwa, waliishi maisha ya furaha ya mume na mke tangu walipofunga ndoa, lakini miaka sita iliyopita hali ilibadilika wakati mumewe alipoacha kutimiza majukumu yake kama mume. Mume wa bibi huyo ni mwalimu mstaafu na Chifu. Mukami alidai mahakamani kuwa matatizo yalianza baada ya Kinyugo kukaa kwa mke mdogo kwa wiki k...
NJOMBE KUONGOZA KWA IDADI YA WATU WANAOISHI NA UKIMWI
Mkoa wa Njombe umetajwa kuongoza kuwa na asilimia 11.4 ya watu wanaishi na virusi vya Ukimwi huku Zanzibar wanaoishi na virusi hivyo ni chini ya asilimia 1. Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk Albina Chuwa ametoa takwimu hizo leo Desemba 1 katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambayo Kitaifa imefanyika viwanja vya Mnazi Mmoja. Dk Chuwa amesema mkoa wa Lindi umekuwa wa mwisho kwa watu wenye virusi vya ukimwi na idadi ya asilimia 0.1 huku maambukizo kwa Jiji la Dar es Salaam yamepungua hadi kufikia asilimia 4.7 ikiwa na maana watu 133,971 wanaishi na ugonjwa huo. Mkurugenzi huyo amesema kwa ujumla watu 1.4 milioni nchini Tanzania wanaishi na virusi vya Ukimwi na takwimu hizo ndiyo rasmi hivyo asitokee mtu au kikundi cha watu kupotosha. "Nasema kwa sababu kuna watu wanakurupuka na kuja na takwimu zao. Naomba watambue takwimu ni fani kama fani nyingine na zina miiko yake," amesema Dk Chuwa Hata hivyo, Dk Chuwa ame...

Maoni
Chapisha Maoni